Consultant and Teaching Hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania
::Bugando Medical Centre
KATIBU MKUU AFYA APONGEZA HUDUMA ZA HOSPITALI YA BUGANDO.
Katibu Mkuu , Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na watoto Dkt.Zainab Chaula leo Oktoba 18, 2019, ameitembelea Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando akiwa ameongozana na wataalamu wa kutoka wizara ya afya,TAMISEMI,Wakurugenzi,waratibu wa program mbalimbali pamoja na baadhi yaviongozi kutoka mkoani.
Dkt. Chaula amesema, Hospitali ya Bugando imekua ikifanya vizuri katika kuboresha huduma zake hivyo imepelekea mapato yake kuongezeka ikiwa inakusanya bilioni 3.8 kwa mwezi hivyo ijikite katika kuboresha zaidi huduma zake katika kusaidia wagonjwa na hivyo amesisitiza wafanyakazi kufanya kazi kwakujituma nakwauadilifu.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Profesa Abel Makubi amesema, Hospitali ya Bugando inaendelea kuboresha huduma zake za kibingwa na kibingwa bobezi katika kuhakikisha mgonjwa anapata huduma bora ikiwa imeboresha huduma za saratani kwa kutoa dawa, tiba mionzi ya ndani na nje,huduma za uchunguzi (CT-SCAN,maabara ya vinasaba na vipimo vya maabara),kukarabati miundombinu,idara ya dharura, vyumba vya upasuaji,mtambo wa oxygen, kiwanda cha maji tiba, na jengo la matibabu ya wagonjwa wanaotumia bima ya afya “One stop Centre”