Consultant and Teaching Hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania
::Bugando Medical Centre
JICHO NI DIRA YA KILA KITU
Hospitali ya Bugando imefanya upimaji wa macho kwa wananchi wa kanda ya ziwa ikiwa imetenga siku tatu kwa ajili ya kuwahudumia wananchi bure.
Mkurugenzi wa upasuaji wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando ,Dkt. Fabian Massaga amesema zoezi hilo la upimaji wa macho limeanza Novemba 19,
2019 linategemewa kuisha Novemba 21,2019 na hivyo kuwaalika wananchi kujitokeza katika zoezi hilo la uchunguziwa macho linalofanyika bure,
mwananchi atachangia kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) za upasuaji tofauti na malipo yakawaida ya hospitali na pia atapata miwani kwa
shilingi elfu tano (5000) ikiwa nikatika kuhakikisha wakazi wa kanda ya ziwa wanapata huduma hii ya macho katika zoezi hili la upimaji.
Dkt. Massaga ameongeza kwa kusema kuwa, “ jicho nidira ya kila kitu, wananchi wengi wanaogopa kufanyiwa upasuaji wa macho kuhofia kuwa
watapata upofu baada ya kufanyiwa upasuaji au wengi wanaita kukwanguliwa” hizo niimani ambazo wananchi wanatakiwa kuachananazo, kwani
kwa sasa madaktari bingwa wa macho wapo nakatika hospitali ya Bugando kuna madaktari bingwawa wa macho wanne (4).Upofu unategemea tatizo
la mgonjwa , tatizo ni kubwa namna gani na amechelewa kufika hospitali, tofauti na angefika hospitali mapema zaidi.
Aidha Dkt. Evarista Mgaya daktari bingwa wamacho, amesema kwa mwaka huu idara ya macho bugando imehudumia takriban wagonjwa wasiopungua
elfu kumi na mbili (12000) wa macho, kati ya wagonjwa hao wengi walikua na shida ya Pressure yamacho, moto wajicho, kisukari nawengine
walihitaji miwani ya kusomea na pia kufanya upasuaji kwa watoto wadogo ambapo mpaka mwezioktoba idara hiyo imefanya upasuaji kwa wagonjwa
mi tisa (900) ambao zaidi ya asilimia tisini (90%) walikua ni wazee ambao wengi walipoteza kuonana baada ya upasuaji walipata kuona tena,
hamsini na sita (56%) walikua ni watoto wa chini ya miaka kumi na tano waliozaliwa na motto wajicho na wengine wamepata mtoto wajicho kwa
sababu ya kuumia. Wengi walihitaji upasuaji lakini asilimia sitini na saba(67%) tu ndio walikubali kufanyiwa upasuaji wengi waliogopa
hawakuafikiwa wasema ukifanyiwa upasuaji jicho lina shindwa kuona tena