Zaidi ya Watu kumi (10) wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanategemea kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe saba hadi kumi na mbili katika Hospitali ya rufaa ya Bugando. Hayo yamesemwa na Prof. William Mahalu mkuu wa kitengo cha Moyo Hospitalini hapa katika kikao na waandishi wa habari. Amesema upasuaji huo unafanyika, kwa ushirikiano wa Madaktari bingwa kutoka Madras Medical Institute ( MMI) Chenai-India, Madaktari wa upasuaji wa moyo wa Hospitali ya Rufaa Bugando pamoja na Daktari Mtanzania ambaye amekuwa mafunzoni Chenai nchini India. Amesema upasuaji huu utahusisha watu wazima wane (4) na watoto sita na wengine ambao watagundulika na matatizo ya moyo yanayohitaji upasuaji.

Katika upasuaji huu wafadhili binafsi wamejitokeza kuchangia safari ya timu hii kutoka Chennai mpaka Tanzania - mwanza, Madaktari hawa wamechangia vifaa vya upasuaji vingi ambavyo vingine wataacha hapa hospitalini kwa ajili ya kuendeleza upasuaji huu. Hata hivyo Prof. Mahalu ameongeza kusema kuwa kitengo cha Moyo wanatarajia kuendelea na upasuaji angalau mara moja kila wiki, kufundisha watu zaidi ili timu ya Hospitalini hapa iwe kubwa na hata kuongeza idadi ya upasuaji kwa wiki na kuendelea kuboresha vifaa.

Naye Rais wa Jumuiya ya Shia Imami Ismaili Muslims kanda ya Magharibi Bw. Altaf Hirani amesema kuwa ujio wa madaktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kwenye Hospitali ya rufaa ya Bugando utasaidia sana katika kuwahudumia wagonjwa wa Moyo kutoka kanda ya ziwa hususani wale ambao wamekuwa wakishindwa kupata matibabu kwa kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu.Hivyo Jumuia hiyo ya Shia imeamua kufadhili kliniki hii ya upasuaji wa Moyo kwa kutambua kuwa, kuwasaidia wenye mahitaji ni sehemu ya maadili yao.

Amesema katika miaka ya hivi karibuni idadi ya wagonjwa wa Moyo nchini Tanzania imekuwa ikiongezeka kwa kasi na matibabu yao yamekuwa yakigharimu kiasi kikubwa cha fedha, na wagonjwa wengi wamekuwa wakisafirishwa kwenda nchi za nje hususani India kwa ajili ya kupata matibabu. Kwa kulitambua hilo, taasisi ya Shia na Hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam imewekeza katika afya ya jamii.

Kwa mwaka 2014 Hospitali ya Ag Khan ilianzisha kitengo cha matibabu ya moyo kwa gharama ya shilingi billion kumi (10) hadi sasa zaidi ya wagonjwa mia sita (600) wamefanyiwa upasuaji wa moyo kwenye kitengo hicho. Na tayari watanzania kumi (10) walipelekwa nchi za nje kwa ajili ya kupata mafunzo. Rais Altaf Hiran ameongeza kuwa Hospitali hiyo pia inatoa mafunzo ya udaktari ikiwa na program ya masomo ya shahada za uzamili katika fani mbalimbali za udaktari, pia Jumuiya hiyo imewekeza shilingi za kitanzania bilioni mia moja sitini na saba ( 167). Vilevile Jumuiya hiyo inatarajia kujenga vituo thelathini na tano (35) vya afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini, na mkoa wa Mwanza vitajengwa vituo vitano (5).

Rais wa Jumuiya ya Shia amewashukuru wadhamini kutoka India kwa kutambua kuwa kuna watanzania ambao wana magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo lakini hawana uwezo wa kifedha wa kugharamia matibabu. Mwisho Prof. Mahalu amewaomba waandishi wa habari kuunga mkono pindi mfuko maalumu wa moyo utakapoanzishwa kwa kuhamasisha jamii kama mchango wao.

The pharmacist focuses on patient care and physician support. This team is centered on providing prescription products, compounds, complementary over-the-counter (OTC) supplies, ..read more..
Saratani ya mlango wa kizazi inazuilika kwa asilimia 100%, Na ikugundulika katika steji ya awali .....soma zaidi..

 

 

One of the patients undergoing intensive medical care in Adult Internsive Care Unit...