BUGANDO MEDICAL CENTRE

Consultant and Teaching Hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania

::Bugando Medical Centre
Wauguzi ni nguvu ya mabadiliko ,huduma bora gharama nafuu .

Ni katika kusherekea siku ya wauguzi duniani tarehe 12/mei ,iliyofanyika kitaifa katika mkoa wa shinyanga, ambapo Hospitali ya Rufaa ya Bugando imeadhimisha siku hii kwa kuwatunuku vyeti baadhi ya wauguzi ambao wamekua wakifanya kazi yao kwa ustadi zaidi ilikuweza kuleta motisha kwa wauguzi wengine katika utendaji kazi wao kwani "wauguzi ni nguvu ya mabadiliko ,huduma bora gharama nafuuā€¯ ikiwa ni kauli mbiu ya siku hii.

Siku hii huadhimishwa kila mwaka kukumbuka siku aliyozaliwa muasisi wa taaluma ya uuguzi duniani Bi Florence Nightingale.

Shughuli hii iliambatana na wauguzi kukumbuka kiapo chao wakiwa wamewasha mishumaa, kazi hii imekua na changamoto kubwa sababu ni ngumu , kwani muuguzi ndio anakaa na mgonjwa kwa muda wote kama walivyoeleza wauguzi hawa kwenye risala yao iliyosomwa na katibu wa chama chao cha TANNA BMC. (TANZANIA NATIONAL NURSES ASSOCIATION).

Bi Asnath Obure kutoka wodi ya Tiba ya Wanaume C7 aliiibuka mshindi kwakua muuguzi bora wa mwaka huu 2015 ambae alipatiwa cheti pamoja na zawadi iliyoandaliwa na chama cha TANNA. Zawadi hizi pia zilitolewa kwa baadhi ya wauguzi kutoka katika wodi mbalimbali ambao wamekua wakifanya kazi zao kwa ustadi.

Akiongea katika sherehe hii Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando Prof. Kien Alfred Mteta akiwa ndie mgeni rasmi wa shughuli hii alisema, Kati ya watumishi 1400 wa Hopitali ya Bugando 500 ni wauguzi hivyo aliahidi kutatua matatizo yao kama walivyoeleza kwenye risala yao ikiwemo malipo kidogo ya kazi za usiku (Night allowance), ucheleweshwaji wa malipo ya sare za kazi (uniform allowance),nyumba za wauguzi kutokua karibu na hospitali,kucheleweshwa wauguzi kupandishwa vyeo,chama cha wauguzi kutokua na ofisi na kutolipwa nauli ya likizo kwa muda.

Mwenyekiti wa TANNA BUGANDO Ibrahimu William Mgoo hakua nyuma kusisitiza kuhusu changamoto wanazopata wauguzi hao ilikuweza kuhakikisha wauguzi wanapata haki zao ili waweze kutoe huduma nzuri kwa wagonjwa.